VIONGOZI MBALIMBALI WATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WINNIE MANDELA
Viongozi mbalimbali
na watu mashuhuri wametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Winnie
Mandela, aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
aliyefariki siku ya jana akiw ana umri wa miaka 81.
![]() |
WINNIE MANDELA |
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema
Winnie alikuwa mwanamke shupavu na imara katika harakati za ukombozi za Afrika
Kusini.
Askofu Mkuu mstaafu wa Afrika Kusini Desmond
Tutu, amesema Winnie ni jasiri katika historia ya vizazi vya wanaharakati
ambaye alikataa kuwasujudia waliomfunga mumewe.
Rais wa Halmashauri
Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema umoja huo unaungana na bara
la Afrika kuomboleza kifo cha Winnie ambaye siku zote atakumbukwa kama
mwanaharakati asiye na woga na aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kupigania
uhuru wa Afrika Kusini na wanawake wote.
Viongozi wengine
waliotoa salama zao za rambirambi ni Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari na
kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga.
VIONGOZI MBALIMBALI WATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WINNIE MANDELA
Reviewed by safina radio
on
April 03, 2018
Rating:
No comments