MKUU WA WILAYA YA MOMBA ATAKIWA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI ANAYESIMAMIA UKARABATI WA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.
TAREHE 17-01-2018
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee
na watoto Mh Dakta Faustine Ndungulile amemwegiza mkuu wa wilaya ya Momba
mkoani Songwe Bw. Juma Ilando kumchukulia hatua za kisheria mkandarasi aliyesimamia
ukarabati wa kituo cha afya cha Tunduma kutokana na kushindwa kusimamia mradi
huo ipasavyo.
Akitoa maagizo hayo mkoani Songwe Mh Ndugulile
amesema kuwa amebaini kuwepo kwa mapungufu mengi katika ukarabati wa kituo
hicho ikiwemo mkandarasi huyo kufanya kazi ya ujenzi bila ramani pamoja na kutumia
shilingi milioni mia moja kujenga msingi peke yake jambo ambalo amelitilia
mashaka.
Mh Ndugulile ametoa wiki mbili kwa mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya hiyo kutoa taarifa ya mpango kazi wa fedha kiasi cha
shilingi milioni mia tano ambazo zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa kituo
hicho.
Mkandarasi huyo ambaye ni Bw Sosypeter Msonja
anadaiwa kushindwa kusimamia ukarabati wa kituo cha afya cha mji mdogo wa
Tunduma ambapo serikali ilitoa kiasi cha shilingi miloni mia tano kwa ajili ya
ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti chumba cha upasuaji pamoja na nyumba ya
mtumishi .
MKUU WA WILAYA YA MOMBA ATAKIWA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI ANAYESIMAMIA UKARABATI WA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.
Reviewed by safina radio
on
January 17, 2018
Rating:

No comments