WAANDAMANAJI SITA NCHINI DRC WAUAWA.
TAREHE 22-01-2018
Waandamanaji sita wameuawa katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kufuatia makabiliano na polisi waliokuwa wakizima maandamano yanayoendelea kusambaa nchini humo kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani.

Polisi wametumia
mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji mjini Kinshasa,ambapo maandamano
kama hayo pia yanaendelea katika miji mingine ndani ya taifa hilo.
Msemaji wa umoja wa
mataifa nchini Jamhuri ya Congo amesema kuwa Zaidi ya watu 50 walijeruhiwa siku
ya jumapili.
Waziri wa zamani Jean
Baptise Sondji ameliambia shirika la habari la AFP kwamba alishuhudia mauaji ya
mtoto mwenye umri wa miaka 16 nje ya kanisa eneo la Kitambo mjini Kinshasa.
Serikali ya Congo
imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote huku siku ya jumamosi mawasiliano ya internet yalikatwa
mjini Kinshasa.
WAANDAMANAJI SITA NCHINI DRC WAUAWA.
Reviewed by safina radio
on
January 22, 2018
Rating:
No comments