MAUTI INAYOSHIKILIA MALANGO YA MIGUU YA WATU HUFANYA KUSHINDWA KUFANIKIWA KIMAISHA.
ARUSHA
12 February, 2018.
![]() |
Waumini wakiwa wamezama katika maombi ya kina katika huduma ya maombi ya radio safina. |
Jamii imetakiwa
kushughulikia roho ya mauti inayoshikilia malango ya miguu ya watu na kuwafanya
kushindwa kufanikiwa kimaisha huku wengine wakikabiliwa na magonjwa sugu na
vifo.
Huduma ya
redio safina kesho katika ukumbi uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili
asubuhi hadi mchana imekuandalia maombi maalumu ya mwendelezo wa kushughulikia
kiapo cha mauti kwenye eneo la malango ya miguu kiroho na kimwili.
Aidha kwa
mujibu wa somo hilo imebainika kuwa wako watu ambao miguu yao imebeba mauti
badala ya amani au hali ambayo inasababisha wao kusongwa na matizo malimbali
kama vile kutokufanikiwa kielimu kiuchumi kiafya na kifamilia kwa ujumla
Pia upo uwezekano wa ndoa kukamatwa na roho ya mauti na
mara nyingine kuwafanya kukosa watoto,kuwa na migogoro isiyoisha, umasikini uliokithiri,
ambapo jamii imeshauriwa kufahamu kuwa njia pekee ya kuondokana na roho hiyo ya
mauti ni kwenda mbele za Mungu kwa
maombi.
Hata
hivyo maombi hayo ya kesho yataambatana na kitendo cha imani cha kuosha miguu
na maji ambayo tayari yameshaombewa kwa kusudi la kufungua miguu ya watu
iliyoshikiliwa kwenye malango ya mauti.
MAUTI INAYOSHIKILIA MALANGO YA MIGUU YA WATU HUFANYA KUSHINDWA KUFANIKIWA KIMAISHA.
Reviewed by safina radio
on
February 12, 2018
Rating:

No comments