NAIBU WAZIRI NYONGO ASEMA KUWA SERIKALI IMEJIPANGA KUDHIBITI MIANYA YOTE YA UTOROSHWAJI WA MADINI .
ARUSHA.
Naibu waziri wa madini
Stanislaus Nyongo amesema kuwa serikali imejipanga kudhibiti mianya y
Mh Nyongo ameyasema
hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kutoka Mikoa
ya Manyara na Arusha kwenye kikao cha kusikiliza changamoto zinazowakabili
wanyabiashara na wachimbaji hao kilichofanyika katika ofisi za madini Kanda ya
Kaskazini Mkoani Arusha.
Amesema kuwa
serikali haifurahii kuona wafanyabiashara na wachimbaji wa madini
wakiumia bali inataka kuweka utaratibu mzuri utakaofanya madini
hayo kuwa na manufaa kwa taifa na kueleza kuwa mpaka sasa mapato
yatokanayo na sekta ya madini hayaridhishi kwani faida yake ni asilimia 04.2 pekee.
Kwa upande wake Naibu
waziri mwenza wa madini Dotto Biteko amesema kuwa lengo la Rais John
Magufuli ni kuona madini hayo yanawanufaisha wananchi wote na kuahidi kuwa
watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wafanyabiashara na wachimbaji hao
wanatoka katika changamoto hiyo na kuwezesha kupanda kwa uchumi wa nchi kupitia
sekta ya madini.
Naye Mwenyekiti wa
chama cha wafanyabiashara na wachimbaji wa madini (TAMIDA) Sammy Mollel
ameeleza kuwa wao kama wafanyabiashara hawataki madini yatoroshwe hivyo
ni vyema serikali ikae nao ili kuweze
kujua ni njia gani watatumia katika kuondokana na changamoto hiyo inayofanya
hali ya biashara ya madini kuwa mbaya.
NAIBU WAZIRI NYONGO ASEMA KUWA SERIKALI IMEJIPANGA KUDHIBITI MIANYA YOTE YA UTOROSHWAJI WA MADINI .
Reviewed by safina radio
on
February 15, 2018
Rating:

No comments