JAFFO ATOA MAAGIZO KWA MAMLAKA ZA MIJI, WILAYA, NA MIJI MIDOGO KUFUNGA DIRA ZA MAJI KWA ASILIMIA 90.
DODOMA.
Taarifa ya Habari 01:00 mchana, 15 February, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh Seleman Jaffo ametoa maagizo kwa mamlaka
za miji, wilaya na miji midogo kufunga dira za maji kwa asilimia 90 hadi ifikapo
mwezi Juni mwaka huu.
Mh Jaffo ametoa maagizo hayo mjini
Dodoma katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji za
miji, wilaya na miji midogo ulioandaliwa na mamlaka ya Udhibiti wa Maji na
Nishati EWURA.
Aidha, Jaffo amesema kuwa katika
kipindi cha miaka tisa (9) mfululizo cha kutoa ripoti ya utekelezaji wa mamlaka
za maji nchini haiwezekani kuona kuwa bado kuna mamlaka ambazo hazijafunga dira
za maji kwa wateja wao.
Hata hivyo, amesema baada ya kipindi
cha miezi sita kupita kama bado kutakuwepo na mamlaka ya maji ambayo haijafunga
dira ya maji atavunja bodi ya mamlaka
hiyo na kumfukuza kazi meneja husika.
JAFFO ATOA MAAGIZO KWA MAMLAKA ZA MIJI, WILAYA, NA MIJI MIDOGO KUFUNGA DIRA ZA MAJI KWA ASILIMIA 90.
Reviewed by safina radio
on
February 15, 2018
Rating:

No comments