Ikulu ya Marekani White House imesema itasubiri kuona hatua za Korea Kaskazini baada ya nchi hiyo kusema iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani, ikiwa ni hatua ya nadra ya kidiplomasia baada ya miezi kadhaa ya Korea kaskazini kurusha makombora na kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia huku kukiwepo na vitisho vya kuanzisha vita kutoka pande zote mbili.
WASHINGTON.
Ikulu ya Marekani
White House imesema itasubiri kuona hatua za Korea Kaskazini baada ya nchi hiyo
kusema iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani, ikiwa ni hatua ya nadra ya kidiplomasia
baada ya miezi kadhaa ya Korea kaskazini kurusha makombora na kufanya majaribio
ya silaha za kinyuklia huku kukiwepo na vitisho vya kuanzisha vita kutoka pande
zote mbili.
![]() |
Msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders |
Msemaji wa White
House Sarah Huckabee Sanders amesema watasubiri kuona hatua za Korea Kaskazini
wakati akiwa katika rasi ya Korea akiwa mmoja wa wajumbe wa Marekani
waliohudhuria michezo ya Olimpiki nchini Korea Kusini.
Ujumbe wa Marekani katika
michezo ya olimpiki uliongozwa na Ivanka Trump, binti wa Rais Donald Trump.
Wakati wa sherehe ya
kufunga michezo hiyo hapo jana, ofisi ya Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ilitangaza
kuwa mjumbe wa Korea Kaskazini aliyehudhuria michezo ya Olimpiki alisema nchi
yake iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani baada ya miongo kadhaa ya
mvutano kati ya nchi hizo mbili, ambazo hazina mahusiano rasmi ya kidiplomasia.
Hata hivyo Trump
aliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini wiki iliyopita.
Ikulu ya Marekani White House imesema itasubiri kuona hatua za Korea Kaskazini baada ya nchi hiyo kusema iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani, ikiwa ni hatua ya nadra ya kidiplomasia baada ya miezi kadhaa ya Korea kaskazini kurusha makombora na kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia huku kukiwepo na vitisho vya kuanzisha vita kutoka pande zote mbili.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:

No comments