MARTIN SCHULZ ATANGAZA KUJIUZULU NAFASI YAKE KAMA KIONGOZI WA CHAMA HICHO.
BERLIN.
Taarifa ya Habari saa 01:00 mchana, 14 February, 2018.
![]() |
Martin Schulz, Kiongozi wa chama cha Social Democratic, SPD. |
Kiongozi wa chama cha Social Democratic,
SPD Martin Schulz ametangaza kujiuzulu mara moja nafasi yake kama kiongozi wa
chama hicho.
Schulz, aliyeshindwa kwenye kinyang'anyiro cha
ukansela na kiongozi wa zamani wa Umoja wa Ulaya alichukua uamuzi wa kujiuzulu
baada ya siku kadhaa za mjadala wa wanachama wa SPD.
Waziri wa zamani wa ajira na kiongozi wa
sasa wa wabunge wa SPD, Andrea Nahles alichaguliwa kuchukua nafasi yake katika
maamuzi ya pamoja ya viongozi wa SPD.
Iwapo atachaguliwa katika mkutano
utakaofanyika katika mji wa Wiesbaden mwezi Aprili, Nahles atakuwa mwanamke wa
kwanza kuongoza, katika historia ya miaka 150 ya chama hicho.
Kulingana na duru za ndani ya SPD Meya wa
Hamburg Olaf Scholz, anayetarajiwa kuwa waziri wa fedha, atakiongoza chama
hicho hadi kitakapofanya mkutano wake Aprili 22.
MARTIN SCHULZ ATANGAZA KUJIUZULU NAFASI YAKE KAMA KIONGOZI WA CHAMA HICHO.
Reviewed by safina radio
on
February 14, 2018
Rating:

No comments