Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ameiagiza taasisi ya kuzua na kupambana na rushwa takukuru hapa nchini kumuhoji aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Masasi Bw Fortunatus Kagoro, pamoja na viongozi wengine kufuatia matumizi mabaya ya fedha ya jengo la utawala wilayani humo.

MTWARA.

Aidha Mh Majaliwa amewataja viongozi wengine wanaokabiliwa na tuhuma hiyo kuwa ni pamoja na Kaimu Mweka hazina wa halmashauri hiyo Heri Hamadi, na Afisa Mipango Bi Teresia Msumba ambao kwa pamoja wanadaiwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha ya Ujenzi wa Jengo la Utawala lililogharimu kiasi cha fedha shilingi bilioni moja na milioni nane.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Wilaya na Halmashauri ya mji wa Masasi ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka madiwani wa halmashauri zote hapa nchini kusimamia fedha za miradi zinazofika katika halmashauri zao ili zitumike vizuri kama zilivyopangwa na serikali.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ameiagiza taasisi ya kuzua na kupambana na rushwa takukuru hapa nchini kumuhoji aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Masasi Bw Fortunatus Kagoro, pamoja na viongozi wengine kufuatia matumizi mabaya ya fedha ya jengo la utawala wilayani humo. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ameiagiza taasisi ya kuzua na kupambana na rushwa takukuru hapa nchini kumuhoji aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Masasi Bw Fortunatus Kagoro, pamoja na viongozi wengine kufuatia matumizi mabaya ya fedha ya jengo la utawala wilayani humo. Reviewed by safina radio on February 26, 2018 Rating: 5

No comments