NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA MH. KANGI LUGOLA AWATAKA WAWEKEZAJI KUFUATA SHERIA.
TAREHE 13-02-2018
![]() |
MH.LUGOLA KUSHOTO |
Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu
wa rais muungano na mazingira Mh Kangi Lugola amewataka wawekezaji wadogo na
wakubwa kufuata sheria na kanuni na mazingira pamoja na matumizi sahihi ya
ardhi ili kulinda afya za wakazi wa maeneo hayo hapa nchini.
Mh Lugola ametoa wito huo wakati wa
ziara yake ya kuzuri kiwanda kidogo kilichopo eneo la Mwangati jijini
Dar-es-salaam,baada ya kupokea malalamiko kuwa kiwanda hicho kipo eneo la
makazi ya watu na kinafanya uchafuzi wa mazingira.
Naye meneja wa kiwanda hicho
kinacholalamikiwa cha Nethin Company Limited Bw Atuman Ramadhan amesema kuwa
amepokea maagizo ya naibu waziri huyo na watayafanyia kazi.
Kwa upande wake mbunge wa Ukonga Mh
Mwita Waitara ameshukuru mwitikio wa naibu waziri huyo kufika katika kiwanda
kinacholalamikiwa na wananchi na kukitolea maelekezo.
NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA MH. KANGI LUGOLA AWATAKA WAWEKEZAJI KUFUATA SHERIA.
Reviewed by safina radio
on
February 13, 2018
Rating:

No comments