JAMII IKISIMAMA VYEMA KATIKA MAOMBI YA UKOMBOZI KWA NJIA YA TOBA NA REHEMA KATIKA ENEO LA NDOA NA MAHUSIANO MUNGU ATACHUKUA NAFASI NA VILIO VYA NDOA, UCHUMI NA AFYA VITAKOMA.
ARUSHA
Imebainishwa kuwa endapo jamii itasimama imara
katika maombi ya ukombozi kwa njia ya Toba na Rehema katika eneo la ndoa na
mahusiano, vilio vya ndoa, uchumi na afya
vitaisha kutokana na Mungu kuchukuwa nafasi.
![]() |
Toba na Rehema. |
Huduma ya redio safina kesho kuanzia saa mbili
asubuhi hadi saa sita mchana katika ukumbi wa maombi ulioko mbauda jijini
Arusha imekuandalia maombi maalumu ya kushughulikia mauti katika ndoa na
uchumba ambayo imeonekana kuwatesa watu wengi katika jamii.
Huduma ya redio safina. |
Aidha kutokana na watu wengi kuendelea kutaabika
katika eneo la ndoa na uchumba imebainika kuwa njia pekee ya kukabiliana na
matatizo hayo ni watu kujikita kwenye maombi ya ukombozi kwa kuomba toba na
rehema mbele za Mungu ili aweze kusamehe
na kuondoa roho hizo zinazowatesa vijana kwenye eneo la uchumba pamoja na
wanandoa.
Shughulikia nguvu ya roho ya mauti ndani ya ndoa katika maeneo tofauti. |
Pamoja na hayo watu mbalimbali wataombewa ili
kufunguliwa kwenye vifungo vinavyowatesa wakiwemo wagonjwa na watu wasiokuwa na
ajira kutokana na kudhibitiwa na roho ya mauti.
JAMII IKISIMAMA VYEMA KATIKA MAOMBI YA UKOMBOZI KWA NJIA YA TOBA NA REHEMA KATIKA ENEO LA NDOA NA MAHUSIANO MUNGU ATACHUKUA NAFASI NA VILIO VYA NDOA, UCHUMI NA AFYA VITAKOMA.
Reviewed by safina radio
on
February 28, 2018
Rating:

No comments