Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote yule atakayekatisha ndoto za mtoto wa kike kwa kumpa ujauzito.



MTWARA.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote yule atakayekatisha ndoto za mtoto wa kike kwa kumpa ujauzito.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa
Mh Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akiendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Mtwara,ambapo amesema kuwa watoto wa kike wanatakiwa kuthaminiwa katika jamii na kuwezeshwa ili waweze kuendelea na masomo bila kubugudhiwa na atakayebainika kumpa mtoto wa kike ujauzito atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kuwa serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike kwa kumpa ujauzito pamoja na kumchukulia hatua kali za kisheria mzazi au mlezi atakayeshiriki kumkwamisha mtoto wa kike kumaliza masomo yake.

Hata hivyo waziri mkuu yupo katika ziara ya siku tatu mkoani Mtwara kiwa anaendelea na zoezi la kukagua miradi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zzinazowakabili wananchi.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote yule atakayekatisha ndoto za mtoto wa kike kwa kumpa ujauzito. Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote yule atakayekatisha ndoto za mtoto wa kike kwa kumpa ujauzito. Reviewed by safina radio on February 27, 2018 Rating: 5

No comments