WAZIRI MKUU WA JAPANI SHINZO ABE AMESEMA KUWA USHIRIKIANO WAKE NA MAREKANI NA KOREA KUSINI NI IMARA
TAREHE 09-02-2018
Waziri Mkuu wa Japan
Shinzo Abe, leo amesema kuwa anataka kutuma ujumbe duniani kwamba ushirikiano
kati ya Marekani, Japan na Korea Kusini kuhusu kitisho cha Korea Kaskazini bado
ni imara.
Abe, ambaye
anatarajiwa kukutana baadaye leo na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, amesema
kabla ya kwenda Pyeongchang katika ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya msimu wa
baridi, kuwa yeye na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence wamesisitiza kuwa
nchi hizo mbili zimesimama pamoja kwa asilimia mia moja.
Hapo jana, kiongozi wa
Korea Kaskazini Kim Jong Un aliongoza maonesho ya kijeshi ambapo maelfu ya
wanajeshi na vifaru waliandaa gwaride, kuadhimisha miongo saba tangu kuundwa
kwa jeshi la nchi hiyo.
Gwaride la kijeshi la Korea Kaskazini
liliandaliwa mara ya mwisho Aprili 2017, na kuoneshwa moja kwa moja kwenye
televisheni.
Korea Kaskazini
inaitumia michezo ya Olimpiki ya Pyeongchang inayoandaliwa Korea Kusini ili
kuanzisha urafiki, ikiwa ni pamoja na kuwatuma watumbuizaji, makundi ya
washangiliaji na dadake Kim Jong Un katika michezo hiyo.
WAZIRI MKUU WA JAPANI SHINZO ABE AMESEMA KUWA USHIRIKIANO WAKE NA MAREKANI NA KOREA KUSINI NI IMARA
Reviewed by safina radio
on
February 09, 2018
Rating:
No comments