WATU 17 WAUAWA KATIKA SHULE MOJA MOJA, FLORIDA, MAREKANI.



WASHINGTON.

Taarifa ya Habari 01:00 mchana, 15 February, 2018.
Wanafunzi Florida wakiwa katika ukaguzi.

Watu 17 wameuawa katika mauaji ya watu wengi yaliyofanywa katika shule moja huko Florida nchini Marekani.

Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo ametajwa kwa jina la Nikolaus Cruz mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikuwa mwanafunzi katika shule hiyo aliyoishambulia.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa amebeba bunduki ya kisasa, alianza kushambulia bila ya mpangilio nje ya shule hiyo kabla ya kushambulia ndani, hali ambayo ilisababisha wanafunzi, kuhangaika huku na kule kwa lengo la kujificha chini ya madawati na maeneo mengine.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo, amesema mshambuliaji huyo kabla ya kushambulia alishafukuzwa shule kutokana na utovu wa nidhamu ambapo polisi wamesema kuwa tayari walimkamata karibu na mji wa jirani wa Coral Springs.

Shirika la Upelelezila la Marekani FBI limesema linashirikiana na polisi, kufanya uchunguzi tukio hilo.

Katika hatua nyingine, kupitia mtandao wake wa Tweeter, Rais Donald Trump amewaondoa hofu raia wa Marekani, kwa kusema kuwa usalama upo wa kutosha kwa mtoto,mwalimu na mwingine yoyote yule.

WATU 17 WAUAWA KATIKA SHULE MOJA MOJA, FLORIDA, MAREKANI. WATU 17 WAUAWA KATIKA SHULE MOJA MOJA, FLORIDA, MAREKANI. Reviewed by safina radio on February 15, 2018 Rating: 5

No comments