KIHAMIA, BILIONI 6.9 ZATENGWA KWA AJILI YA KUTEKELEZA MIRADI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI.
ARUSHA.
Taarifa ya habari saa 08:00 usiku, 13 February, 2018.
![]() |
Bw Athumani Kihamia Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha |
Jumla ya Fedha shilingi bilioni 6.9 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kuwahudumia wananchi hususani katika sekta ya elimu,afya na miundombinu ya barabara.
Hayo yameyasemwa Bw Athumani
Kihamia Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha katika kikao maalum cha
Kamati ya Maendeleo ya Wilaya kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha
2016/17 na bajeti mpya ya halmashauri ya jiji la Arusha kilichofanyika katika
ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali.
Kihamia amesema kuwa vikao
vya mapendekezo ya bajeti na watendaji wa kata,viongozi wa dini,makundi ya
wazee na vijana tayari vimeshaanza ili kupata maoni yao yatakayo wawezesha
katika kutatua changamoto za wananchi iwapo zitatekelezwa kama walivyopanga.
Aidha amesema kutokana na
ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
baadhi ya wajumbe wamependekeza kuwekwa kwa kipaumbele cha ujenzi wa madarasa
ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani jambo ambalo litasaidia kuboresha
maendeleo ya taaluma shuleni.
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Gabriel Dakaro ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inajenga
madarasa yaliyobaki yapatayo 771 ambayo yatagharimu kiasi cha fedha shilingi
bilioni 4.4 ifikapo mwezi Novemba mwaka huu hadi kukamilika ili kuweza
kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa uliopo kwa sasa.
Kwaupande wake Naibu Meya
wa Jiji la Arusha Viola Lazaro amesema kuwa hulka ya baadhi ya watendaji
kushughulikia tatizo la uhaba wa madarasa na kipindi ambacho kina idadi kubwa
ya wanafunzi wanaojiunga na masomo ya sekondari kimekuwa kikiwagharimu watoto
kushindwa kufanya vizuri kitaaluma kutokana na msongamano wa wanafunzi uliopo.
KIHAMIA, BILIONI 6.9 ZATENGWA KWA AJILI YA KUTEKELEZA MIRADI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI.
Reviewed by safina radio
on
February 13, 2018
Rating:

No comments