Serikali imetoa wiki mbili kwa mwekezaji wa shamba la mifugo la Kafoi Estate Wilayani Siha West Kilimanjaro kukamilisha mpango kazi wa uendelezaji wa shamba hilo kwa kuwa hajafikia matakwa ya mkataba huo kutokana na ongezeko la ng’ombe.
KILIMANJARO.
Serikali imetoa wiki mbili kwa mwekezaji wa shamba
la mifugo la Kafoi Estate Wilayani Siha West Kilimanjaro kukamilisha mpango kazi
wa uendelezaji wa shamba hilo kwa kuwa hajafikia matakwa ya mkataba huo kutokana
na ongezeko la ng’ombe.
![]() |
Waziri wa Kilimo na UvuviLuhaga Mpina. |
Muda huo wa wiki mbili umetolewa na Waziri wa Kilimo
na Uvuvi Luhaga Mpina baada ya mwekezaji wa shamba hilo linalohudumia na
kuzalisha ng’ombe wa maziwa na nyama kutoa takwimu kuwa shamba hilo lina ng’ombe
mia tatu takwimu ambazo si za kweli.
Aidha, Waziri Mpina amesema mwekezaji huyo
amejitungia takwimu zake kwa kusema kuwa kuna ng’ombe 300 wakati wako ng’ombe
168 huku akihoji kuhusiana na kutoa taarifa hizo za uongo kwa serikali.
Katika hatua nyingine Mh. Mpina ameitembelea Ranchi ya
Taifa NARCO na kuagiza uongozi wa Ranchi hiyo kuwa na mifugo kulingana na
ukubwa wa shamba na ukarabati wa miundombinu ili kukidhi mahitaji ya shamba
hilo.
Hata hivyo, amesema kuwa serikali imeipa mwaka mmoja
NARCO kuanzia mwezi January hadi Desemba kuhakikisha kuwa mashamba yote yana
mifugo kulingana na ukubwa wake pamoja na kuhakikisha kuwa miundombinu yote iliyochakaa
inafufuliwa sambamba na mashamba kuwa na mifugo ya kutosha ili NARCO itekeleze
ufugaji bora kwa kuwa ni kioo cha ufugaji.
Ziara ya Waziri Mpina ya siku mbili katika mikoa ya
Arusha na Kilimanjaro inakamilika wilayani Siha kwa kutembelea taasisi za
wizara, kukagua utendaji kazi, na kupokea madume kumi na moja katika kituo cha
taifa cha uzalishaji mbegu bora za mifugo.
Serikali imetoa wiki mbili kwa mwekezaji wa shamba la mifugo la Kafoi Estate Wilayani Siha West Kilimanjaro kukamilisha mpango kazi wa uendelezaji wa shamba hilo kwa kuwa hajafikia matakwa ya mkataba huo kutokana na ongezeko la ng’ombe.
Reviewed by safina radio
on
February 27, 2018
Rating:

No comments