Waziri wa elimu sayansi na teknolojia na mafunzo ya ufundi Prf. Joyce Ndalichako amekitaka Chuo Kikuu cha Maount Meru cha jijini Arusha kuacha utaratibu wa kutoa alama za makisio kwa wanafunzi kwani serikali haitasita kukifunga chuo hicho kutokana na utaratibu huo.



ARUSHA.

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia na mafunzo ya ufundi Prf. Joyce Ndalichako amekitaka Chuo Kikuu cha Maount Meru cha jijini Arusha kuacha utaratibu wa kutoa alama za makisio kwa wanafunzi kwani serikali haitasita kukifunga chuo hicho kutokana na utaratibu huo.

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia na mafunzo ya ufundi Prf. Joyce Ndalichako.
Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea chuo hicho na kuona namna kinavyosimamia utoaji wa elimu ya juu na kuongeza kuwa wizara yake imeshatoa maagizo kupitia Tume ya Vyuo Vikuu nchini kuwaondoa wahadhiri ambao hawana sifa za kufundisha lakini agizo hilo mpaka sasa halijatekelezwa.

Aidha, Waziri Ndalichako amesema kuwa ili wanafunzi hao waweze kutambulika na kuweza kuajiriwa ndani ya Tanzania inatakiwa mitihani yao isahihishwe au kuangiliwa na watu wa nje ili alama za matokeo hayo yatumike.

Pia, Waziri ndalichako ameongeza kuwa endapo suala hilo halitawezekana, wanafunzi hao wanatakiwa kufanya mtihani na kusahihishwa ili kuondokana na tatizo hilo la kukisia alama za matokeo pamoja na kuondoa suala hilo kwa lengo la kutokuharibu mfumo wa elimu ya Tanzania.

Kwa upande, wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mount Meru Dk. Masau Kituka ameeleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya wanafunzi kuwa ni makosa ya walimu na si wanafunzi.

Hata hivyo, udahili wa wanafunzi katika chuo hicho cha Mount Meru mpaka sasa umesitishwa hadi kitakapo rekebisha kasoro zilizopo.



Waziri wa elimu sayansi na teknolojia na mafunzo ya ufundi Prf. Joyce Ndalichako amekitaka Chuo Kikuu cha Maount Meru cha jijini Arusha kuacha utaratibu wa kutoa alama za makisio kwa wanafunzi kwani serikali haitasita kukifunga chuo hicho kutokana na utaratibu huo. Waziri wa elimu sayansi na teknolojia na mafunzo ya ufundi Prf. Joyce Ndalichako amekitaka Chuo Kikuu cha Maount Meru cha jijini Arusha kuacha utaratibu wa kutoa alama za makisio kwa wanafunzi kwani serikali haitasita kukifunga chuo hicho kutokana na utaratibu huo. Reviewed by safina radio on February 26, 2018 Rating: 5

No comments