KAMISHNA MUSLIM, ASKARI WENYE TOCHI MAALUMU WATAKUWAPO KILA KILOMITA MOJA KATIKA ENEO LA KIBUKU.
TANGA.
Polisi kitengo cha usalama barabarani
kimesema kuwa kila kilometa moja eneo la Kabuku ilipotokea ajali ya watu watano
itakuwa na askari wenye tochi maalumu na watafanya hivyo baada ya kubaini kuwa
eneo hilo ni eneo korofi.
Mkuu wa operesheni,Kikosi cha usalama
barabarani nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Muslim
ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea eneo la Kibuku kuona namna ajali
zinavyoweza kudhibitiwa .
Aidha, Kamanda Muslim amesema kuwa
katika kipindi cha miezi miwili Januari hadi sasa ajali mbili zimetokea eneo la
Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga na kugharimu maisha ya watu kumi na
wengine kadhaa kuijeruhiwa.
Amesema amefika katika eneo hilo ili
kuona kilichotokea na kuweza kukagua eneo la tukio ambapo tukio hilo lilitokea
tarehe 21 mwezi Januari mwaka huu iliyohusisha ajali ya Noah hivyo kutokana na
matukio hayo katika eneo hilo linaonesha eneo hilo kuwa ni hatarishi.
Hata hivyo, mapema wiki hii ajali za
barabarani katika eneo hilo la Kibuku limesababisha vifo vya watu watano na
wengine sita kujeruhiwa.
KAMISHNA MUSLIM, ASKARI WENYE TOCHI MAALUMU WATAKUWAPO KILA KILOMITA MOJA KATIKA ENEO LA KIBUKU.
Reviewed by safina radio
on
February 15, 2018
Rating:

No comments