UNHCR IMESEMA MIONGONI MWA WATU 11 WALIOUAWA NCHINI RWANDA WATANO NI WAKIMBIZI KUTOKA CONGO.
TAREHE 27-02-2018
![]() |
BAADHI YA ASKARI WA KULINDA USALAMA |
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa
(UNHCR) limesema miongoni mwa watu 11 waliouliwa Alhamis iliyopita nchini
Rwanda, watano walikuwa ni wakimbizi kutoka Congo.
Afisa wa shirika hilo Daniela Lonita amesema vifo
hivyo vilitokea katika kambi ya wakimbizi ya Kiziba pamoja na mji wa karibu wa Kibuye magharibi mwa Rwanda.
Maelfu ya
watu walikuwa wamekwenda kuandamana katika ofisi za Shirika la Mpango wa
Chakula la Umoja wa Mataifa, baada ya shirika hilo kupunguza ugawaji wa chakula
kwa asilimia 10 mwezi Novemba na kwa asilimia 25 kuanzia Januari.
Polisi ya Rwanda imethibitisha vifo vya watu watano
pekee katika taarifa yake ya Ijumaa iliopita iliosema kwamba ilichukua hatua
baada ya waandamanaji kuwajeruhi maafisa wa polisi saba kwa kutumia mawe,
viboko na vyuma.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa unaisisitiza serikali ya
Rwanda kulifanyia uchunguzi tukio hilo.
UNHCR IMESEMA MIONGONI MWA WATU 11 WALIOUAWA NCHINI RWANDA WATANO NI WAKIMBIZI KUTOKA CONGO.
Reviewed by safina radio
on
February 27, 2018
Rating:

No comments