MAKAMU RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKIZINDUA MRADI WA REGRO.


IRINGA.
12 February, 2018.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani akiwa Iringa kwaziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan hii leo amezindua mradi wa kuimarisha Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini mwa Tanzania ujulikanao kama REGRO.
Mh. Samia amezindua mradi huo ikiwa ni siku yake ya nne ya Ziara ya kikazi mkoani Iringa ambapo amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea jumla ya fedha kiasi cha dola milioni 150 kutoka Benki Kuu ya Dunia kwa ajili ya kutekeleza mradi wa miaka sita.
Aidha, Amesema kuwa lengo la mradi huo ni kukuza utalii na kipato cha wananchi kwa kuboresha miundombinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija.
Pia amewaasa watendaji wa Taasisi zitakazotekeleza mradi huo kuwa waadilifu kusimamia mradi huo mkubwa ili kufikia malengo yanayotarajiwa kwa kuwa mkopo huo utalipwa na watanzania wote hivyo amewakumbusha kutumia fedha hizo katika shughuli zilizokusudiwa.
Wakati huo huo, Mh Samia amekutana na kuzungumza na wananchi wa manispaa ya Iringa ambapo amesema kilimo cha korosho ni fursa nyingine ya kukuza kipato na ni zao linalofanya vizuri kwa sasa huku mikoa ya Dodoma, Morogoro ikichangamkia kulima zao hilo hivyo amewaasa wananchi wanaopakana na Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma waanze kulima zao hilo.
Hata hivyo, amesema kuwa huduma za afya,maji na umeme zitaendelea kuboreshwa ambapo amewataka wananchi kukataa maambukizi ya virusi vya UKIMWI huku akiwaagiza watendaji wa serikali kuendelea kuimarisha utawala bora, miundombinu ya reli na barabara.

MAKAMU RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKIZINDUA MRADI WA REGRO. MAKAMU RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKIZINDUA MRADI WA REGRO. Reviewed by safina radio on February 12, 2018 Rating: 5

No comments