Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Bi Mary Tesha amewataka wazazi na walimu kutoa ushirikiano kwa malezi ya watoto wao ili kuwakinga na mimba za utotoni.
MWANZA.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Bi Mary
Tesha amewataka wazazi na walimu kutoa ushirikiano kwa malezi ya watoto wao ili
kuwakinga na mimba za utotoni.
![]() |
Bi Mary Tesha |
Akiwa katika ziara ya kutembelea shule za sekondari wilayani humo Bi Tesha ametoa rai kwa wanaokatisha ndoto za wanafunzi wa kike ili watoto waweze kusoma hadi kumaliza elimu yao.
Bi. Tesha amesema tatizo la mimba za utotoni kwa
wanafunzi wengi hasa wa kike limekuwa kikwazo kwa watoto cha kufikia malengo ya
kielimu kwa kukatiza ndoto zao kusoma huku wakijikuta wakilea watoto katika
umri mdogo.
Aidha, Bi Tesha amesema kuwa anataka wanaume
wanaowapa watoto hao wa kike mimba wakamatwe na kushtakiwa kwa ajili ya sheria kuchukua
mkondo wake ili wanaume watakapowaona
watoto wa kike wawaogope badala ya kumchukua mtoto huyo wa kike akiwa na mimba
na kumchunguza, kumkamata pamoja na kuhangaika naye.
Hata hivyo, Bi. Tesha ameongeza kuwa endapo hatua
hizo zikichukuliwa kwa wanaume hao watawaogopa watoto wa shule na itatoa
uhakika kwa watoto wa kike kusoma shule pamoja na kumaliza tatizo la mimba za utotoni .
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Bi Mary Tesha amewataka wazazi na walimu kutoa ushirikiano kwa malezi ya watoto wao ili kuwakinga na mimba za utotoni.
Reviewed by safina radio
on
February 28, 2018
Rating:

No comments