Watu wanne wameuawa na wengine wanne wamelazwa hospitalini baada ya mlipuko ulioambatana na moto kuharibu jengo la ghorofa tatu katika mji wa Leicester nchini Uingereza.
MANCHESTER.
Watu wanne wameuawa na wengine wanne wamelazwa
hospitalini baada ya mlipuko ulioambatana na moto kuharibu jengo la ghorofa
tatu katika mji wa Leicester nchini Uingereza.
Chanzo cha mlipuko huo uliotokea usiku wa kuamkia
leo hakijajulikana, lakini polisi wanasema kisa hicho hakihusishwi na ugaidi.
Wakaazi wa
eneo hilo la mkasa wamesema majumba yao yalitikiswa na mlipuko huo
uliosababisha moto mkubwa.
Afisa
msimamizi wa eneo hilo Shane O’Neill amesema wanaamini huenda kuna watu ambao
hawajapatikana na hivyo juhudi za uokozi zinaendelea.
Watu wanne wameuawa na wengine wanne wamelazwa hospitalini baada ya mlipuko ulioambatana na moto kuharibu jengo la ghorofa tatu katika mji wa Leicester nchini Uingereza.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:
No comments