Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wataalamu wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Lindi LUWASA kukaa Kwenye kituo cha kusukuma maji kilichopo kwenye mradi wa maji wa Ng`apa ili kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kusababisha wananchi wa mji wa Lindi kukosa maji.



LINDI.

Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wataalamu wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Lindi LUWASA kukaa Kwenye kituo cha kusukuma maji kilichopo kwenye mradi wa maji wa Ng`apa ili kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kusababisha wananchi wa mji wa Lindi kukosa maji.

Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe.

Mhandisi Kamwelwe ameyasema hayo alipotembelea mradi wa maji wa Ng’apa na kubaini tatizo la umeme linalowasababisha wananchi wa mji huo kukosa maji mara kwa mara.

Amesema kuwa katika eneo hilo umeme unakuja usiku na kusababisha bomba hilo la maji kufumuka zaidi ya mara tatu jambo ambalo si la kawaida ikilinganishwa na maeneo mengine ya Ruvu juu na Ruvu chini mkoani Pwani.

Hata hivyo mradi wa maji wa Ng’apa unahudumia zaidi ya wakazi elfu themanini na tano katika mji wa Lindi ambapo waziri huyo amabaini tatizo la umeme kukatika mara kwa mara na wakati mwingine kutokuwepo nyakati za usiku na kukosekana kwa mtu wa kuwasha pampu za kusukuma maji hali inayosababisha kero kubwa kwa wakazi wa mji huo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Lindi Bw Shaibu Ndamanga ameishukuru serikali kwa uamuzi wake wa kubeba jukumu la kugharamia umeme kwenye mradi huo na hiyo itasaidi kuondoa tatizo la umeme katika kituo hicho.

Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wataalamu wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Lindi LUWASA kukaa Kwenye kituo cha kusukuma maji kilichopo kwenye mradi wa maji wa Ng`apa ili kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kusababisha wananchi wa mji wa Lindi kukosa maji.  Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wataalamu wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Lindi LUWASA kukaa Kwenye kituo cha kusukuma maji kilichopo kwenye mradi wa maji wa Ng`apa ili kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kusababisha wananchi wa mji wa Lindi kukosa maji. Reviewed by safina radio on February 27, 2018 Rating: 5

No comments