SERIKALI ITACHUKUA HATUA YA KUIMARISHA MAHAKAMA KWA LENGO LA KUTOA HAKI KWA WANANCHI KWA WAKATI, DK. ALLY MOHAMED SHEIN.


ZANZIBAR.

12 February, 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ally Mohamed Shein katika sherehe ya siku ya sheria Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ally Mohamed Shein amesema kuwa serikali itachukua hatua ya kuimarisha mahakama kwa lengo la kutoa haki kwa wananchi kwa wakati.

Dr Sheikn ametoa kauli hiyo wakati akizungiumza katika siku ya sheria Zanzibar katika ukumbi wa zamani wa baraza  la wawakilishi Kikwajuni Visiwani Zanzibar, ambapo amesema kuwa wananchi wanajenga imani na serikali iwapo misngi ya sheria itafuatwa na mahakama na kuwa huru bila kuingiliwa katika utendaji wake.

Ameongeza kuwa utawala wa sheria ndio dira ya mafanikio wa mpango mkuu wa serikali katika kuwaletea wanachi maendeleo katika sekta zote za kiuchumi na kijamii pamoja na kudumisha amani na utulivu.

Amefafanua kuwa utaratibu huo utawezesha Zanzibar kutekeleza mpango wa kuimarisha viwanda,utalii,kuvutia wawekezaji,mfumo mzuri wa kibiashara,kuendeleza kilimo,uvuvi na ufugaji wa kisasa pamoja na uhifadhi wa mazingira.

Hata hivyo Dr Shekn ameitaka mahakama kutumia mfumo wa  TEHEMA ili kuongeza ufanisi na tija katika mfumo wa utatuzi wa migogoro na kesi nyingine mbalimbali.

SERIKALI ITACHUKUA HATUA YA KUIMARISHA MAHAKAMA KWA LENGO LA KUTOA HAKI KWA WANANCHI KWA WAKATI, DK. ALLY MOHAMED SHEIN. SERIKALI ITACHUKUA HATUA YA KUIMARISHA MAHAKAMA KWA LENGO LA KUTOA HAKI KWA WANANCHI KWA WAKATI, DK. ALLY MOHAMED SHEIN. Reviewed by safina radio on February 12, 2018 Rating: 5

No comments