WAZIRI JAFO ATOA RAI KWA JAMII NCHINI KUUNGA MKONO MPANGO WA SERIKALI WA ELIMU BURE
TAREHE 08-02-2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh. Dk. Suleman Jaffo ametoa rai kwa jamii nchini
kuunga mkono mpango wa serikali wa kutoa elimu bure kwa kujitolea vifaa vya
kujifunzia ili kuwawezesha wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uhitaji
kupata elimu bora.
Waziri Jaffo ametoa rai hiyo wakati wa uzinduzi wa
mpango wa kusaidia vifaa vya kijifunzia kwa watoto wanaotoka katika familia
zisizo na uwezo uliofanyika katika shule ya msingi ya Ukuzi wilayani Chamwino mkoani
Dodoma.
Waziri Jaffo ameeleza kuwa kutokana na ukosefu wa
fursa ya vitendea kazi hivyo vya elimu kwa watoto wanaotoka katika familia zenye
uhitaji, jamii imewakosa watoto wenye maarifa.
Aidha, amesema kuwa wanafunzi hao wanaotoka katika
familia zenye uhitaji husoma na kupata elimu yao katika hali ya majonzi hivyo
jamii kwa pamoja inapaswa kuwaunga mkono wote wanaojitokeza katika kuunga mkono
mpango huo wa kutoa elimu bure kwa kujitolea vifaa vya kujifunzia.
Naye Kaimu Afisa wa Elimu wilaya ya Chamwino Abraham
Msigwa amesisitiza suala la kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika
kuwawezesha wanafunzi namna ya kujifunza huku baadhi ya wanafunzi wakikiri kuwa
vifaa vya kujifunzia ni changamoto miongoni mwao.
WAZIRI JAFO ATOA RAI KWA JAMII NCHINI KUUNGA MKONO MPANGO WA SERIKALI WA ELIMU BURE
Reviewed by safina radio
on
February 08, 2018
Rating:

No comments