Rais wa Urusi, Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kuhusu machafuko ya nchini Syria.



MOSCOW.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kuhusu machafuko ya nchini Syria.


Rais wa Urusi, Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa Ikulu ya rais wa Urusi, katika mazungumzo yao, viongozi hao wameangazia umuhimu wa jitihada za pamoja kuutekeleza mkataba wa kusitisha mashambulizi kwa siku 30 uliopitishwa na Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema, Merkel na Macron wamemhimiza Putin kuongeza shinikizo zaidi kwa utawala wa Syria kusitisha mashambulizi ya angani na mashambulizi mengine Ghouta Mashariki.

Taarifa imesema Merkel, Macron na Putin wameukubali uamuzi wa Umoja wa Mataifa hasa kuruhusu misaada kufikishwa na kuondolewa kwa watu katika eneo la vita.

Hata hivyo Wamesisitiza kuwa kusitishwa kwa mashambulizi kutawezesha kuanzishwa kwa juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa.


Rais wa Urusi, Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kuhusu machafuko ya nchini Syria. Rais wa Urusi, Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kuhusu machafuko ya nchini Syria. Reviewed by safina radio on February 26, 2018 Rating: 5

No comments