WAPIGANAJI 10 WA ANSAR DINE WAUAWA KUTOKANA NA SHAMBULIO LA ANGA KUTOKA JESHI LA UFARANSA.
BAMAKO.
![]() |
Ndege ya kivita ya ufaransa ikiparuka kwa ajili ya mashambulizi ya anga nchini dhidi ya kundi la Kiislamu la Ansar Dine. |
Wapiganaji wasiopungua 10 wa kundi la Kiislamu la Ansar Dine wameuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Ufaransa wakati wa operesheni iliyokua ikimlenga kiongozi wa kundi hilo,Bw Iyad Ag Ghaly nchini Mali.
vyanzo vya usalama vimethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Jeshi la Mali (FAMA) Siku ya Jumatano usiku lilibaini kuwa Mshirika wa karibu wa kiongozi huyo, afisa wa zamani aliyetoroka jeshi la Mali, aliuawa katika mashambulizi hayo.
Ansar Dine, washirika wa Al Qaeda, ni sehemu ya makundi ya waasi yanayodhibiti eneo la kaskazini mwa Mali kati ya mwaka 2012 na Januari 2013.
Kwa mujibu wa yanzo vya kijeshi Mnamo mwaka 2015, baada ya kikosi cha Ufaransa cha Barkhane kutokomeza,kuua au kukamata mamia ya wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa Mali,Bw Iyad Ag Ghaly alikimbilia kwenye mpaka wa Algeria.
Chanzo cha usalama katika ripoti iliyotolewa imebaini kwamba wapiganaji wa Ansar Dine kati ya 10 hadi 17 waliuawa katika mapigano hayo.
WAPIGANAJI 10 WA ANSAR DINE WAUAWA KUTOKANA NA SHAMBULIO LA ANGA KUTOKA JESHI LA UFARANSA.
Reviewed by safina radio
on
February 15, 2018
Rating:

No comments