KISIWA CHA TONGA KIMEPIGWA NA KIMBUNGA NA KUSABABISHA MAFURIKO MAKUBWA.


TAREHE 13-02-2018


Kimbunga Gita kinachoorodheshwa kuwa cha kiwango cha nne kimepiga kisiwa cha Tonga ambacho ni miongoni mwa visiwa vya bahari ya Pasifiki mapema hii leo na kusababisha mafuriko makubwa pamoja na kuharibu mifumo ya umeme.

Maafisa wa nchi hiyo wanakielezea kimbunga Gita kuwa ni kikali zaidi kuwahi kupiga mji mkuu wa kisiwa hicho, Nuku'alofa.

Kimbunga hicho kimekipiga kisiwa cha Tonga na kusababisha uharibifu mkubwa kutokana na upepo mkali wa kiasi cha mwendo wa kilomita 233 kwa saa, na kuharibu takribani asilimia 40 ya makazi katika mji huo mkuu.

Hakukua na taarifa yoyote ya vifo vilivyosababishwa na dhoruba hiyo, lakini wengi wamejeruhiwa, baadhi yao vibaya.

Visiwa vingine vilivyopo bahari ya Pasifiki pia vitapigwa na kimbunga Gita wakati kikielekea Fiji, Vanatu na New Caledonia katika siku chache zijazo.

KISIWA CHA TONGA KIMEPIGWA NA KIMBUNGA NA KUSABABISHA MAFURIKO MAKUBWA. KISIWA CHA TONGA KIMEPIGWA NA KIMBUNGA NA KUSABABISHA MAFURIKO MAKUBWA. Reviewed by safina radio on February 13, 2018 Rating: 5

No comments