JUMLA YA WALIMU 105 WILAYANI KARAGWE WAMELIPWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MIA TANO
TAREHE 07 FEB 2018
Jumla walimu 105 wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wamelipwa zaidi ya shilingi milioni mia tano kutokana na malimbikizo ya madeni ya mishahara yao pamoja na kupandishwa vyeo bila ya kurekebishiwa mishahara.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh Joseph Kakunda wakati alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa aliyetaka kujua serikali italipa lini malimbikizo ya mishahara ya waalimu katika wilaya ya Karagwe.
Amesema kuwa Serikali imekuwa ikilipa malimbikizo ya madeni ya mishahara ya walimu kila mwezi kupitia akaunti zao za benki ambapo hadi kufikia Juni 30 mwaka jana serikali imelipa zaidi ya shilingi bilioni 14 kwa walimu elfu kumi na nane mia nane tisini na tano kati ya shilingi bilioni 69.461 zilizokuwa zikidaiwa hadi kipindi cha mwaka fedha wa 2015/2016.
Hata hivyo, amebainisha kuwa serikali imeendelea kuimarisha Tume ya ya Utumishi wa Walimu-PFC kwa kuipatia Ofisi ya Makao makuu, ofisi za wilaya, pamoja na kuipatia samani za ofisi na watumishi kama vile Ofisi ya PFC wilayani Karagwe ambayo ina Katibu wa Wilaya na watumishi wawili.

Reviewed by safina radio
on
February 07, 2018
Rating:

No comments