Mpango wa usitishaji mapigano wa kila siku unaoruhusu usambazaji wa misaada ya kiutu, uliotangazwa na Urusi umeanza kufanya kazi siku ya Jumanne katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Ghouta Mashariki karibu na mji mkuu wa Damascus Syria, kufuatia wimbi la mashambulizi ya angani na mabomu yaliyoendelea usiku kucha.
DAMASCUS.
Mpango wa usitishaji
mapigano wa kila siku unaoruhusu usambazaji wa misaada ya kiutu, uliotangazwa
na Urusi umeanza kufanya kazi siku ya Jumanne katika eneo linaloshikiliwa na
waasi la Ghouta Mashariki karibu na mji mkuu wa Damascus Syria, kufuatia wimbi
la mashambulizi ya angani na mabomu yaliyoendelea usiku kucha.
Mkuu wa shirika la uangalizi wa haki za
binadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman, amesema mpango huo umeanza kufanya
kazi hii leo na kuna utulivu katika maeneo yote ya Ghouta mashariki.
Kwa mujibu wa wizara
ya ulinzi ya Urusi Usitishaji huo wa muda katika maeneo ya mapambano umeanza
saa tatu asubuhi na unatarajia kudumu hadi saa sita mchana kila siku.
Njia ya usambazaji wa
misaada ya kiutu itawekwa ili kuwaruhusu raia kuondoka katika eneo hilo.
Mpango wa usitishaji mapigano wa kila siku unaoruhusu usambazaji wa misaada ya kiutu, uliotangazwa na Urusi umeanza kufanya kazi siku ya Jumanne katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Ghouta Mashariki karibu na mji mkuu wa Damascus Syria, kufuatia wimbi la mashambulizi ya angani na mabomu yaliyoendelea usiku kucha.
Reviewed by safina radio
on
February 27, 2018
Rating:

No comments