MAGAIDI 23 WA AL-SHABAB WAUAWA NA JESHI LA KENYA KWA KUSHIRIKIANA NA SOMALIA LIMEUA
MOGADISHU.
Jeshi la Kenya likishirikiana na Jeshi la Somalia, limewauwa
magaidi 23 wa Al Shabab katika mji wa Fahfahdun Kusini Magharibi mwa mkoa wa
Gedo nchini Somalia.
![]() |
Jeshi la Kenya likishirikiana na Jeshi la Somalia, limewauwa magaidi 23 wa Al Shabab katika mji wa Fahfahdun |
Ripoti zinasema magaidi hao waliuawa wakati wanajeshi wa Kenya
chini ya mwavuli wa AMISOM walipokuwa wanafanya oparesheni ya kulenga ngome
mpya za magaidi hao.
Makabiliano makali yalishuhudiwa kwa muda wa saa nne kati ya
wanajeshi wa AMISOM na magaidi hao waliokuwa wamejihami kwa silaha hatari.
Majeshi ya Kenya KDF na yale ya Somalia SDF, yanasema mbali na
mauaji hayo, walifanikiwa kuwapokonya magaidi hao silaha na kuteketeza moto
magari kadhaa pamoja na kambi yao.
Kenya
ilituma jeshi lake nchini Somalia mwaka 2011, baada ya Al Shabab kuwateka nyara
wafanyikazi wawili wa Kihispania waliokuwa wanalifanyia kazi Shirikila la
Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, katika kambi ya Daadab nchini Kenya
MAGAIDI 23 WA AL-SHABAB WAUAWA NA JESHI LA KENYA KWA KUSHIRIKIANA NA SOMALIA LIMEUA
Reviewed by safina radio
on
February 28, 2018
Rating:

No comments