KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA ANTONIO GUTERRES AITAKA SERIKALI YA MALDIVES KUONDOA HALI YA HATARI.

TAREHE 07-02-2018
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka serikali ya Maldives kuondoa hali ya hatari na kuhakikisha usalama wa raia wake wakiwemo watumishi wa idara ya mahakama.

Wito huo umejiri baada ya rais wa Maldives Abdullah Yameen, kutangaza hali ya hatari na vikosi vyake vya usalama kuivamia mahakama ya juu.

Aidha, Jaji Mkuu wa mahakama hiyo pamoja na jaji mwingine wamekamatwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu huyo Stephane Dujarric imesema kuwa Guterres anaisihi serikali ya Maldives kuheshimu katiba na utawala wa sheria kuondoa amri ya hali ya hatari haraka iwezekanavyo na kuchukuwa hatua zote kuhakikisha usalama wa watu nchini humo.

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi kuhusu hali inayojitokeza nchini Maldives na hasa tangazo la hali ya hatari na hatua ya vikosi vya usalama kuingia katika eneo la mahakama.  

Hata hivyo, katika hotuba yake kwa taifa rais Yameen amewatuhumu majaji kwa kuwa sehemu ya njama ya kumpindua.



KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA ANTONIO GUTERRES AITAKA SERIKALI YA MALDIVES KUONDOA HALI YA HATARI. KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA ANTONIO GUTERRES AITAKA SERIKALI YA MALDIVES KUONDOA HALI YA HATARI. Reviewed by safina radio on February 07, 2018 Rating: 5

No comments