Waendesha mashtaka wa Korea Kusini wanataka rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun Hye ahukumiwe katika kesi ya ufisadi ambayo ilisababisha yeye kuondolewa madarakani.



SEOUL.

Waendesha mashtaka wa Korea Kusini wanataka rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun Hye ahukumiwe katika kesi ya ufisadi ambayo ilisababisha yeye kuondolewa madarakani.

Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun Hye.
kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na shirika la habari la Yonhap,Park alikutwa na hatia Aprili 18 mwaka jana kwa makosa kadhaa ya ufisadi ikiwemo rushwa, matumizi mabaya ya madaraka,na kuvujisha siri za serikali.

 Rais huyo wa zamani hakutokea katika mahakama mjini Seoul wakati wa kesi yake leo Jumanne.

Park ambaye alikuwa ni rais wa kwanza mwanamke wa Korea Kusini, alituhumiwa kwa kumpa nafasi kubwa rafiki yake wa karibu Choi Soon Sil ya kufanya biashara na serikali licha ya ukweli kwamba Choi hakuwa na ofisi rasmi.

Rais huyo wa zamani aliwekwa kando na mahakama ya kikatiba ya Korea Kusini mwezi Machi baada ya kuondolewa madarakani kwa kashfa za rushwa kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya kumtaka ajiuzulu.

Waendesha mashtaka wa Korea Kusini wanataka rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun Hye ahukumiwe katika kesi ya ufisadi ambayo ilisababisha yeye kuondolewa madarakani. Waendesha mashtaka wa Korea Kusini wanataka rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun Hye ahukumiwe katika kesi ya ufisadi ambayo ilisababisha yeye kuondolewa madarakani. Reviewed by safina radio on February 27, 2018 Rating: 5

No comments