ASKARI TANO WA JESHI LAPOLISI WAMEUAWA NA KUNDI LA WTU WENYE SILAHA KATIKA MASHAMBULUZI DHIDI YA KITUO CHA POLISI KUKO AFRIKA KUSINI.
PRETORIA.
Askari watano wa Jeshi la polisi wameuawa na kundi la watu
katika mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi katika mji mdogo kusini mashariki
mwa Afrika Kusini leo Jumatano.
![]() |
Jeshi la polisi Afrika Kusini wakifanya uchunguzi baada ya tukio l;a mauaji ya askari tano kuawa na watu wenye silaha. |
Kundi la watu wenye silaha walifanya mashambulizi dhidi ya kituo
cha polisi cha Engcobo katika mkoa wa Cape mashariki usiku wa kuamkia leo.
Habari zinaeleza kuwa kundi hilo liliwafyatulia risasi polisi hao
na kuwashikilia mateka wawili miongoni mwao.
Msemaji wa polisi Vish Naidoo ameliambia shirika moja la habari
la AFP kuwa,leo asubuhi na mapema, watu sita waliuawa wakati genge la wezi
lilipofanya mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi.
Msemaji huyo wa polisi ameongeza kuwa watu watano kati ya sita
waliouawa walikuwa polisi, ambapo watu watatu walipigwa risasi katika kituo cha
polisi baada ya wezi hao kufyatua risasi kiholelea.
Mashambulizi dhidi ya polisi yanafanyika mara kwa mara nchini
Afrika Kusini, ambayo inavunja rekodi kwa viwango vya juu zaidi vya uhalifu
duniani ambapo takwimu rasmi zinaeleza kuwa Maafisa wa polisi wasiopungua 57
waliuawa wakiwa kazini kati ya mwezi Aprili 2016 na mwezi Machi 2017.
ASKARI TANO WA JESHI LAPOLISI WAMEUAWA NA KUNDI LA WTU WENYE SILAHA KATIKA MASHAMBULUZI DHIDI YA KITUO CHA POLISI KUKO AFRIKA KUSINI.
Reviewed by safina radio
on
February 21, 2018
Rating:

No comments