MKUCHIKA, MFUKO WA RAIS KUJITEGEMEA ILI KUTOA HUDUMA NCHINI KOTE.
DAR-ES-SALAAM.
Taarifa ya Habari saa 08:00 usiku, 13 February, 2018.
![]() |
Kaptein George Mkuchika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Ututumishi wa Umma na Utawala Bora. |
Waziri wa nchi ofisi ya rais Menejimenti ya
Ututumishi wa Umma na Utawala Bora Kaptein George Mkuchika amesema kuwa serikali
itatekeleza azma ya bunge ya kutaka mfuko wa rais wa kujitegemea kutoa huduma
nchini kote.
Akizungumza na Watumishi wa Mfuko huo jijini
Dar es salaam Mh. Mkuchika amesema kuwa baadhi ya watu wanakosa fursa ya maendeleo
kwa kuwa huduma za mfuko huo hazifiki nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mfuko huo Haigati Kitala amesema
kupitia mfuko huo wananchi wengi wamepata hari na mwamko ya kuanzisha miradi ya
maendeleo.
Hata hivyo, kwa sasa mfuko wa rais wa
kuwezesha wananchi kiuchumi unafanya shughuli zake kwa mikoa ya Dar es salaam,
Iringa, na Morogoro.
MKUCHIKA, MFUKO WA RAIS KUJITEGEMEA ILI KUTOA HUDUMA NCHINI KOTE.
Reviewed by safina radio
on
February 13, 2018
Rating:

No comments