RAMAPHOSA ASEMA KUWA HATIMA YA RAIS JACOB ZUMA ITAJULIKANAQ SIKU CHACHE ZIJAZO.
TAREHE 08-02-2018
Mwenyekiti Taifa wa chama tawala cha ANC
cha Afrika Kusini amesema kuwa, hatima ya Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo
itajulikana siku chache zijazo.
Mwenyekiti huyo ambaye ni Bw Cyril
Ramaphosa amesema kuwa, tayari ameanza mazungumzo na Rais Jacob Zuma kuhusiana
na suala la kukabidhi madaraka na masuala mengineyo.
Ameongeza kuwa, matokeo ya mazungumzo
yao yatajulikana siku chache zijazo na wakati huo ndipo itajulikana hatima ya
Rais Jacob Zuma.
Ramaphosa ambaye pia ni Makamu wa Rais
wa Afrika Kusini amesema, mazungumzo yake na Jacob Zuma yalikuwa mazuri na
yamechunguza njia bora na za haraka za kutatua matatizo ya nchi hiyo.
Rais Jacob Zuma amezidi kuwa chini ya
mashinikizo ya chama tawala cha ANC tangu Cyril Ramaphosa alipochaguliwa
kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Iwapo Jacob Zuma atajiuzulu, Cyril
Ramaphosa ambaye ni makamu wake atachukua uongozi wa Afrika Kusini hadi
utakapoitishwa uchaguzi mwingine wa rais mwaka 2019.
RAMAPHOSA ASEMA KUWA HATIMA YA RAIS JACOB ZUMA ITAJULIKANAQ SIKU CHACHE ZIJAZO.
Reviewed by safina radio
on
February 08, 2018
Rating:

No comments