WATU 15 WAMEUAWA NCHINI CONGO DRC
TAREHE 28-02-2018
Watu wasiopungua 15 wameuawa katika wimbi jipya la mapigano katika eneo la Kasai huko Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.
![]() |
ASKARI WA KONGO |
Watu wasiopungua 15 wameuawa katika wimbi jipya la mapigano katika eneo la Kasai huko Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.
Andre Kapiola, chifu wa eneo la Lombelu mkoani Kasai
amesema askari mmoja wa serikali na wapiganaji 14 wa kundi la waasi wa Kamwina
Nsapu wameuawa katika mapigano hayo mapya.
Mkoa wa Kasai umekuwa uwanja wa makabiliano kati ya jeshi la
serikali na waasi wa Kamwina Nsapu, kiongozi wa kikabila aliyeuawa na
maafisa usalama mnamo Septemba mwaka 2016.
Kundi la Kamwina Nsapu lilianzisha harakati hizo kupinga hatua
ya Rais Joseph Kabila kuendelea kung'ang'ania madaraka licha ya muhula wake
kisheria kumalizika.
Haya yanajiri katika hali ambayo, watu 22 waliuawa baada
ya kundi la waasi wa Nyatura ambao aghalabu yao wanatoka kabila la Wahutu
kuvamia vijiji vya Kalusi na Bwalanda na kukabiliana na waasi wa
genge la Mai Mai Mazembe siku ya Jumapili na Jumatatu iliyopita.
Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo yanashuhudia machafuko na mapigano kwa zaidi ya miaka 20
sasa.
WATU 15 WAMEUAWA NCHINI CONGO DRC
Reviewed by safina radio
on
February 28, 2018
Rating:

No comments