Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ametoa muda wa wiki moja kwa Halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha kuwa zinapata na kusambaza mabomba na sumu za kuulia wadudu wanaoshambulia zao la pamba.
TAREHE 28-02-2018
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ametoa
muda wa wiki moja kwa Halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha kuwa
zinapata na kusambaza mabomba na sumu za kuulia wadudu wanaoshambulia zao la
pamba.
![]() |
MKUU WA MKOA WA SINGIDA REHEMA NCHIMBI |
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo wilayani Iramba
baada ya wakulima kulalamikia suala la ukosefu wa dawa na mabomba ya kupulizia sumu
ya kuulia wadudu wanaoshambulia zao hilo.
Wakulima hao wamedai kuwa kabla ya kupata elimu hiyo
hawakupata elimu sahihi kutoka kwa wataalamu na hivyo kusababisha mimea yao
kuendelea kushambuliwa na wadudu licha ya kupulizia sumu ya kuulia wadudu hao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ametoa muda wa wiki moja kwa Halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha kuwa zinapata na kusambaza mabomba na sumu za kuulia wadudu wanaoshambulia zao la pamba.
Reviewed by safina radio
on
February 28, 2018
Rating:

No comments