BOMU LA VITA YA PILI YA DUNIA YASITISHA SAFARI ZA NDEGE LONDON, UNGEREZA.

LONDON.
12 February, 2018.
Uwanja wa ndege wa Uingereza.

Uwanja wa ndege wa mjini London umefungwa baada ya bomu la vita vya pili vya dunia kupatikana kwenye mto ulio karibu wa Thames nchini humo.

Uwanja huo utafungwa siku nzima na safari zote za ndege kufutwa, ambapo utawaathiri zaidi ya abiri elfu kumi.

Bomu hilo liligunduliwa siku ya Jumapili eneo la George wa (5) V wakati wa shughuli ya kikazi mashariki mwa London.

Uwanja huo ukafungwa nhuku polisi wakisema kuwa wanashirikiana na jeshi la wanamaji kuondoa bomu hilo.

Abiria wameambiwa wasisafiri kwenda uwanja huo na kushauriwa kuwasiliana na mashirika yao ya ndege.

BOMU LA VITA YA PILI YA DUNIA YASITISHA SAFARI ZA NDEGE LONDON, UNGEREZA. BOMU LA VITA YA PILI YA DUNIA YASITISHA SAFARI ZA NDEGE LONDON, UNGEREZA. Reviewed by safina radio on February 12, 2018 Rating: 5

No comments