ZAIDI YA WANAFUNZI 80 WAKOSA MAHALI PA KULALA MVAVANI, NJOMBE.
NJOMBE.
Zaidi ya wanafunzi 80 wa shule ya sekondari ya
Mvavani katika halmashauri ya wilaya ya mji wa Makambako mkaoni Njombe hawana
mahali pa kulala baada ya bweni lao kuteketea kwa moto hapo jana.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Makambako
wwanafunzi hao wamesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme
iliyotokea katika bweni hilo ambapo hawakuweza kuokoa kitu chochote.
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.
Christopher Ole Sendeka amesema kuwa kamati ya kuchunguza chanzo cha moto huo
itaundwa kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kujua sababu
iliyosababisha mabweni hayo kuteketea kwa moto.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk. Christopher Ole Sendeka. |
Naye Mkuu wa Shule hiyo Mwl Tude Mahenge
amewashukuru wasamaria wema kwa jitihada walizoonesha pamoja na misaada mingine
wanayoitoa shuleni hapo.
ZAIDI YA WANAFUNZI 80 WAKOSA MAHALI PA KULALA MVAVANI, NJOMBE.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments