RAIS WA MYNMAR AJIUZULU


Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Myanmar inasema kuwa Rais wa nchi hiyo  Htin Kyaw amejiuzulu.

Kiongozi wa Myanmar mwenye mamlaka Aung Suu kyi na rais wa taifa hilo Htin Kyaw kulia
RAIS WA MYNMAR HTIN KYAW KULIA




Image captioHakuna sababu iliyotolewa lakini kumekuwa na wasiwasi katika miezi ya hivi karibuni kuhusu afya ya rais huyo mwenye umri wa miaka 71 baada ya kuonekana amedhoofikaKyaw aliapishwa kuwa rais 2016 baada ya uchaguzi uliositisha miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi.Lakini alikuwa kiongozi asiye na mamlaka huku aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Aung San Suu Kyi akiwa kiongozi mwenye mamlaka.
Makamu wa rais Myint Swe , jenerali wa zamani atakuwa kaimu rais hadi pale rais mpya atakapochaguliwa katika muda wa siku saba sijazo, taarifa hiyo ilisema.

RAIS WA MYNMAR AJIUZULU RAIS WA MYNMAR AJIUZULU Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments