NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MH. ABDALAH AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mh Abdalah Ulega
ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kwa kuweka mikakati
dhabiti ya kupambana na uvuvi haramu.
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mh Abdalah Ulega |
Mh Ulega ametoa pongezi hizo alipokuwa katika ziara
ya kukagua mwalo wa Miyobozi uliko wilayani Uvinza mkoani humo ambapo amesema
kuwa jitihada hizo za wilaya zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza
mapato ya halmashauri na serikali.
Aidha naibu waziri huyo amesisitiza suala la mapambano
dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa rasilimali za uvuvi ambapo amewaagiza wakazi
wa wilaya ya Uvinza kuacha utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Ameongeza kuwa fedha nyingi zimeekezwa katika mwalo
wa Miyobozi na kutaka wavuvi katika eneo hilo kutumia vizuri mwalo huo ambao
una hadhi ya kimataifa kwani kwa mwaka
wa fedha uliopita mwalo huo ulichangia kiasi cha shilingi milioni 28.
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MH. ABDALAH AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA
Reviewed by safina radio
on
March 19, 2018
Rating:
No comments