SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA VYANZO VYA MAJI YAPELEKEA VYANZO HIVYO KUPOTEZA UWEZO WA KUZALISHA MAJI NA KUHATARISHA USALAMA WA MAJI.
Imeelezwa kuwa uhifadhi wa mazingira
katika nyanzo vya maji bado ni changamoto kubwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jambo ambalo linapelekea
vyanzo vya maji kupoteza uwezo wa kuzilisha maji na kuhatarisha usalama
wa maji.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi. |
Akisoma Taarifa ya hiyo mbele ya
Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi wakati wa maadhimisho
ya wiki ya Maji iliyofanyika katika Kijiji cha Seloto Kata ya Dareda
Mhandisi wa maji wa Halmahauri hiyo Bw Samweli Tluway amesema kumekuwa
na shughuli nyingi za kibinadamu katika vyanzo vya maji.
Amesema kuwa uchafuzi na uharibifu
wa vyanzo vya maji unasababishwa na shughuli za kilimo
zinazofanyika kwenye vyanzo vya maji, uchungaji wa mifugo,ujenzi wa
makazi ya kuishi, ujenzi wa vyoo pamoja na ukataji miti na utengenezaji
wa mkaa ndani ya vyanzo vya maji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo
Raymond Mushi amesema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kutunza vyanzo vya maji
na kupanda miti maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji na kutokufanya
shughuliz zinazoweza kuathiri vyanzo vya maji hususani kilimo na
ufugaji.
Amesema kuwa hali ya maji
inaridhisha lakini haijafikia kiwango kinachotakiwa hivyo watu wote
kwa ujumla wanapaswa kutambua umuhimu wa maji katika maisha yao hivyo ni
muhimu kushirikiana kutunza vyanzo hivyo ili viwasaidie.
SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA VYANZO VYA MAJI YAPELEKEA VYANZO HIVYO KUPOTEZA UWEZO WA KUZALISHA MAJI NA KUHATARISHA USALAMA WA MAJI.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments