WAKAZI WAYAKIMBIA MAKAZI YAO, GHOUTA MASHARIKI KARIBU NA MJI MKUU WA SYRIA, DAMASCUS.
Maelfu ya raia wameukimbia mji wa Ghouta Mashariki nchini Syria
baada ya mwezi mzima wa mfulululizo wa mashambulizi ya vikosi vya Serikali
ambavyo vinakaribia kuudhibiti kabisa mji huo kutoka kwa waasi nje kidogo ya
jiji la Damascus.
Baadhi ya waokoajia na watu wakizidi kukimbia kutokana na mashambulizi yanayoendelea. |
Rais wa Bashar al-Assad ameendelea kujiimarisha madarakani
wakati huu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vikiingia mwaka wa nane.
Assad ameendelea kusisitiza kuwa mashambulizi hayo yataendelea
hadi pale ngome hiyo ya upinzani inayosalia itakapoangushwa huku vikosi vyake
vikiwa vimefanikiwa pakubwa katika vita vya kuuchukua mji wa Ghouta ambao
wakati fulani ulikuwa ngome kuu ya wapiganaji waasi.
Waangalizi wa masuala ya vita wanasema kuwa kwa sasa vikosi vya
Syria vimefanikiwa kushikilia asilimia 70 ya mji huo na kuwagawa wapiganaji
waasi katika makundi matatu ambayo hayana uwezo tena wa kukabiliana na vikosi
vya Serikali na washirika wake nchi ya Urusi.
Waangalizi wa haki za binadamu wanasema idadi ya raia
waliokimbia ndani ya siku moja kutoka kwenye mji huo ni kubwa zaidi kuwahi
kushuhudiwa katika historia ya vita vya Syria.
WAKAZI WAYAKIMBIA MAKAZI YAO, GHOUTA MASHARIKI KARIBU NA MJI MKUU WA SYRIA, DAMASCUS.
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments