TRUMP, , AMTEUA LARRY KUDLOW, MCHAMBUZI WA MASUALA YA FEDHA KUWA MSHAURI MPYA WA MASUALA YA UCHUMI KATIKA IKULU YA WHITE HOUSE.
WASHINGTON.
Rais Donald Trump wa Marekani
amemteuwa Mchambuzi wa masuala ya fedha katika televisheni nchini Marekani,
Larry Kudlow kuwa mshauri mkuu mpya wa masuala ya uchumi katika Ikulu ya
Marekani ya White house.
Rais Donald Trump.
Kudlow amelieleza shirika la habari la AP kuwa
amekubaliana na uteuzi huo wa rais Donald Trump kuhudumu kama mshauri wa
masuala ya uchumi.
|
Kudlow atachukua nafasi ya Gary
Cohn ambaye alitangaza wiki iliyopita kuwa atajiuzulu nafasi hiyo baada ya
kupinga mipango ya rais Donald Trump inayohusiana na viwango vipya vya kodi
kibiashara.
Kudlow mwenye umri wa miaka 70 ni
mchambuzi mwandamizi katika kituo cha Televisheni cha CNBC.
TRUMP, , AMTEUA LARRY KUDLOW, MCHAMBUZI WA MASUALA YA FEDHA KUWA MSHAURI MPYA WA MASUALA YA UCHUMI KATIKA IKULU YA WHITE HOUSE.
Reviewed by safina radio
on
March 15, 2018
Rating:
No comments