TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA ISRAEL ILI KUIMARISHA JESHI LA ULINZI


Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussen Mwinyi amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali ya Israel katika kuimarisha jeshi la ulinzi la wananchi Tanzanaia  JWTZ ili liweze kukabiliana na vitendo vya kiuhalifu na ulinzi wa amani.


Image result for PICHA YA HUSSEIN MWINYI WAZIRI WA ULINZI
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussen Mwinyi

Dr Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Dar-es-salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya siku tatu hapa nchini ya waziri wa ulinzi wa Israel Azegdo Lebaman,ambapo amesema kuwa JWTZ imekuwa na ushirikiano na Israel ambayo inasaidia mafunzo mbalimbali ya kijeshi kwa maafisa wa jeshi la JWTZ.

Amesema kuwa wamekuwa wakijifunza mafunzo mbalimbali kutoka Israel ikiwemo mapambano dhidi ya ugaidi,uharamia,na vita vinavyoitwa vya kisasa hivyo ni matumaini yao kuwa ziara hiyo itafungua milango ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel.

Kwa upande wake waziri wa ulinzi wa Israel Azegdo Lebaman amesema kuwa kwa sasa watatoa mafunzo ya ulinzi kwa kutumia tekinolojia ya Tehama na namna ya kufanya uchunguzi katika matukio mbalimbali ya kiuhalifu.


TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA ISRAEL ILI KUIMARISHA JESHI LA ULINZI TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA ISRAEL ILI KUIMARISHA JESHI LA ULINZI Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments