WATANZANIA WATAKIWA KUFANYIA USAFI VINYWA VYAO
Ikiwa kesho ni maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa
duniani jamii imetakiwa kufanyia usafi vinywa vyao ikiwa ni pamoja na
kuhudhuria katika kiliniki za vinywa na meno ili kupima afya zao.
Ushauri huo umetolewa na Dr Christian Maria ambaye
ni mratibu wa afya ya kinywa katika
halmashauri ya Meru wakati akizungumza na Redio Safina kuhusu maadhimisho ya
siku ya kinywa ambayo kitaifa itafanyika mkoani Mara.
Dr Maria amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa
wakisumbuliwa na matatizo ya kinywa kutokana na kutofanyia usafi vinywa vyao hivyo
wanatakiwa kutumia dawa ya meno yenye floride ambayo inasaidia kuimaraisha meno
na fizi.
Aidha amewataka wananchi kuhudhuria katika kiliniki
za vinywa na meno ili kupima afya zao ili kama watabainika kuwa na matatizo
waanze matibabu mapema na kupata ushauri.
Amesema kuwa katika kuadhimisha siku hiyo
halmashauri ya wilaya ya Meru imejipanga kutoa huduma ya kinywa kwa watoto wapatao
elfu kumi na sita mia tatu na kumi na nane wenye mahitaji maalumu kutoka katika shule 60 za msingi za serikali kuanzia
chekechea hadi darasa la tatu.
Hata hivyo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya afya
ya kinywa duniani kwa mwaka huu ni SEMA HA FIKIRIA KINYWA FIKIRIA AFYA.
WATANZANIA WATAKIWA KUFANYIA USAFI VINYWA VYAO
Reviewed by safina radio
on
March 19, 2018
Rating:
No comments