8,592 YAELEZWA KUWA NI IDADI YA WAKIMBIZI WA ETHIOPIA KUINGIA KENYA.
NAIROBI.
Kamati ya msalaba
mwekundu ya Kenya imetoa taarifa ikisema hadi sasa idadi ya wakimbizi wa
Ethiopia waliokimbilia nchini humo imefikia elfu nane na miatano tisini na
mbili tangu tarehe 10 mwezi huu, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.
Taarifa hiyo imesema
kuwa kamati ya msalaba mwekundu ya Kenya imewapatia wakimbizi hao chakula na
huduma za afya, na wamepewa hifadhi katika wilaya ya Moyale ya kaunti ya
Marsabit na eneo la Sololo karibu na mpaka wa nchi hizo mbili, kaskazini mwa
Kenya.
Pia taarifa hiyo
imesema vikosi vya Ethiopia viliwashambulia raia kwa makosa tarehe 10 mwezi huu
kwenye eneo la Moyale lililoko karibu na mpaka kati ya Ethiopia na Kenya, na
kusababisha vifo vya raia tisa na wengine 12 kujeruhiwa.
Kikosi hicho cha
jeshi la Ethiopia kiliwashambulia raia hao wakidhani kuwa ni waasi wa kundi la
upinzani Oromo Libertation Front hali iliyowasababisha baadhi ya raia wa
Ethiopia kukimbilia nchini Kenya.
Hadi sasa kazi ya
kuandikisha wakimbizi bado inaendelea.
8,592 YAELEZWA KUWA NI IDADI YA WAKIMBIZI WA ETHIOPIA KUINGIA KENYA.
Reviewed by safina radio
on
March 15, 2018
Rating:
No comments