14 WAFA NA WENGINE KADHAA WAJERUHIWA KUTOKANA NA MLIPUKO NJE YA HOTELI, MOGADISHU, SOMALIA.
Watu 14 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa siku ya Alhamisi wakati gari lilipolipuka nje ya hoteli moja maarufu mjini Mogadishu, Somalia.
Kundi la kigaidi la Al-Qaeda. |
Msemaji wa Serikali amesema watu 14 walipoteza maisha kwenye eneo la tukio na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka wakati huu vikosi vya uokoaji vikiendelea kutafuta miili zaidi.
Watu walioshuhudiwa tukio hilo wanasema mlipuko huo ulitokea kwenye mtaa wa Makkah al-Mukarama moja ya mitaa ambayo inashughuli nyingi kuunganisha na eneo la kati la mji wa Mogadishu.
Mji wa Mogadishu umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na kundi la Al-Shabab linalopigana kuiangusha Serkali ya Somalia inayotambuliwa kimataifa.
14 WAFA NA WENGINE KADHAA WAJERUHIWA KUTOKANA NA MLIPUKO NJE YA HOTELI, MOGADISHU, SOMALIA.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments