KAMWELWE AAGIZA MAMLAKA ZOTE ZA MAJI KULIPIA MAJI KWA MAMLAKA ZA MABONDE YA MAJI KAMA WANANCHI WANAVYOLIPIA MAJI WANAYOYATIBU.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Izack Kamwelwe
ameziagiza Mamlaka zote za Maji Nchini kulipia maji wanayoyachukua katika
Mamlaka ya Mabonde ya Maji hatua ambayo itachangia utunzaji wa vyanzo vya maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe. |
Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo mkoani Mbeya
alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi na Bodi ya Mamlaka ya Maji na Mazingira la
jiji la Mbeya.
Aidha, Kamwelwe amezitaka mamlaka hizo kulipia maji
wanayoyachukua kutoka vyanzo vya maji kwa kila mwezi kwa kuwa wananchi
wanayalipia maji hayo wanayoyatibu, kwa ajili ya matumizi ya majumbani na
viwandani.
Pia, amesema kuwa lazima Mamlaka hizo ziweze
kushiriki katika kuchangia kutunza vyanzo vyanzo vya maji kutokana na kulipia
maji hayo wanayochukua katika mabonde ya maji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Safu za Mazingira
Mlima Mbeya Venance Awela pamoja na Afisa Maji Bonde la Ziwa Rukwa Grace
Kitanda wamesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji ni mzuri lakini wanakabiliwa
na shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji.
Akiwa ziarani mjini Mbeya mbali na mambo mengine
Waziri Mhandisi Kamwelwe ameweka jiwe la msingi katika ofisi mpya za Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya.
KAMWELWE AAGIZA MAMLAKA ZOTE ZA MAJI KULIPIA MAJI KWA MAMLAKA ZA MABONDE YA MAJI KAMA WANANCHI WANAVYOLIPIA MAJI WANAYOYATIBU.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments